Rais Samia alionyesha moyo wa
unyenyekevu na huruma kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025, kwa kutoa pole za
dhati kwa wale wote walioathirika.
"Nimehuzunishwa sana na
tukio lile. Natoa pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu na jamaa. Tunaomba
Mungu aziweke roho zao mahali pema. Kwa majeruhi, tunawaombea wapone haraka, na
kwa waliopoteza mali, tunawaomba wawe na stahamala na uvumilivu,” alisema Rais
Samia.
Katika mahojiano na wadau
mbalimbali baada ya hotuba ya Rais Samia
yenyen lengo la uponyaji na kuzuka kwa kauli mbalimbali nchini kuhusu ni nani
au nini kinakuwa kikwazo ya safari hiyo, wamnesema ni kibri na ubinafsi.
Mfanyabiashara wa Tanga Bw. Rashid Mwinyi "Demon (kikwazo) wetu mkubwa ubinafsi.
Bila Amani Hakuna Maendeleo! Utulivu ndio Uzalendo wa Kweli."
Mch. Neema Mwasonga wa Mbeya
anasema : "Kikwazo ni roho ya kutoamini katika taasisi zetu. Tunaona maoni
mengi katika matandao kama 'ohh Tumeunda Tume Nyingi Sana Hazijawahi Kuja Na
Majibu'. Si kweli majibu yapo ni lazima Watanzania waiunge mkono serikali kwa
imani kuwa hekima na utulivu vipo kwa viongozi wetu, na tutafanikiwa."
Mkazi mmoja wa Dar es Salaam Dkt.
Imani Kileo anasema : "Wale
wanaokwamisha ni wanaochochea chuki kwa kutumia mitandao na wanaokataa kulegeza
misimamo yao ya kisiasa na ya kiimani. Rais anataka maridhiano, lakini wengine
wanatafuta 'Mbuzi wa Bwana Kheri' wa kulaumu badala ya kuvaa jezi moja ya
TANZANIA."
Mjasirimali wa Arusha Bi. Stela
Mushi "Anasema kikwazo ni kushindwa
kuona mbali. Vurugu zimerudisha nyuma biashara zetu. Bila Amani Hakuna
Maendeleo! Tusiangalie tofauti zetu ndogo ndogo. Tuvuke hayo. Tufanye Kazi,
Tukue Haraka!"
Kauli ya Rais Samia kuhusu
msamaha na pole inaweka msingi wa kihisia na kimaadili kwa uponyaji. Hata
hivyo, wajibu wa uponyaji wa taifa si wa Rais pekee, bali ni wa kila Mtanzania.
Kama inavyosisitizwa katika jumbe
mbalimbali, siri ya kufika mbali haraka sio ngumu: ni kila Mtanzania kukubali
kuwa Wote Pamoja, Kazi Iende Haraka! Tofauti zetu zikiwekwa kando, tunaweza
kukabiliana na shida yetu ya
kutokuaminiana na urasimu.
Kwa kumuunga mkono kiongozi wetu
kwa vitendo, na kufanyia kazi maelekezo yake, tunaweza kutimiza malengo ya
taifa na kuhakikisha tunavuka salama. Umoja na mshikamano katika kujenga taifa
letu ndio dira.

0 Maoni