Hasara kubwa ya kiuchumi imeripotiwa kufuatia
vurugu, huku wananchi wa hali ya chini wakikosa hata riziki ya siku na kuingia
kwenye madeni, jambo linaloonesha wazi umuhimu wa amani kama msingi wa maisha.
Kipindi cha Lockdown kimeacha maumivu ya muda mrefu.
kijana mmoja ambaye hakupoenda kutaja jina lake
anaeleza athari za moja kwa moja za kukosekana kwa amani na maandalizi hafifu
ya kukabiliana na majanga ambayo yanatokea kwa kushtukiza.
"Ile lockdown imetusababishia madeni manake
hatukuwa na chochote, kwanza tulikuwa hatuitarajii kutokea yale yaliyotokea.
Pili, tunakuwaga hatuna akiba familia zetu nyingi. Wengine ndio tumetoka jana;
sio siku tano, wengine tuna siku sita na wengine saba. Tudumishe amani, amani
ndio kila kitu."
Faizat Peter, mkazi na mfanyabiashara wa Mbagala,
anaeleza athari za kijamii na kiuchumi: "Kiufupi maandamano yalituathiri
kiuchumi na kifamilia kiujumla. Maisha ya Mtanzania asilimia kubwa ni utoke ili
upate kuishi. Watu wamepata taabu, familia zimeathirika, kulingana na kipato
imekuwa taabu sana."
Mtaalamu wa Uchumi wa Familia anasema, "Familia nyingi za Watanzania
huishi kwa mapato ya siku. Kukaa ndani kwa siku tano hadi saba kunamaanisha
wamepoteza mapato yote. Tunapaswa kujifunza kutokana na hili, tutaweza
kudumisha utulivu wa kiuchumi kwa kuwa katika utaratibu, tusigeuze
utaratibu" alisema.

0 Maoni