Mgombea Ubunge Jimbo la
Bukombe kupitia Chama Cha Mapunduzi (CCM) Dkt. Doto Mashaka Biteko amewashukuru
wana Bukombe kwa heshima waliyompa kipindi chote Cha kampeni Katika wilaya ya
Bukombe.
Dkt. Biteko ametoa
shukurani hizo Oktoba 27, 2025 wakati wa kuhitimisha kampeni Katika Uwanja wa
Igulwa, Wilayani Bukombe, Mkoani Geita.
"Nataka niwaambie
wana Bukombe huwa mnanipa deni kubwa sana moyoni mwangu hamjui tu, huwa hamjui
huwa najiona mmenipa stahili nisiyostahili kwa sababu kama binadamu nina
mapungufu yangu mengi lakini mnanipa heshima," amesema Biteko.
Dkt. Biteko
amewashukuru pia vijana wa hamasa na kuahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali.
"Nitafanya kila
linalowezekana vijana wa hamasa wasiishie Kwenye kampeni ni vijana wetu lazima
tuwakomboe. Nataka niwaambie kila wakati tukiwaita mnakuja mnanipa deni na
heshima kubwa sana."
Aidha, Dkt. Biteko
amewakumbusha wana Bukombe Kuwa leo ilikuwa siku ya kuhitimisha kampeni katika
jimbo la Bukombe na tarehe 29 wajiyokeze kwa wingi vituoni kupiga kura kwa
wagombea wote wa CCM Ili Chama hicho kiendelee Kuwa madarakani.




0 Maoni