Mabadiliko katika sekta ya nishati yanaonekana
dhahiri kote nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Mkoa wa Shinyanga
unakaribia kuwa kituo kipya cha nishati safi, nafuu, na endelevu, huku mradi
mkubwa wa kuzalisha umeme kwa kutumia JUA (Solar Power Project) ukikaribia
kukamilika.
Taarifa mpya zimeonyesha kuwa mradi huu wa kimkakati
umefikia hatua ya asilimia 78.5 (78.5%) ya ujenzi. Katika awamu yake ya kwanza,
mradi unatarajiwa kuzalisha jumla ya megawati 50 za umeme.
Gharama ya mradi huu inafikia kiasi cha Shilingi
Bilioni 323, ikiashiria uwekezaji mkubwa wa Serikali unaolenga kuimarisha
upatikanaji wa nishati kwa wananchi na kukuza uchumi wa viwanda.
Nguvu ya Jua, Nguvu ya Maendeleo
Kukamilika kwa mradi huu kunatarajiwa kupunguza
utegemezi wa vyanzo vya nishati vinavyochafua mazingira na kukuza matumizi ya
nishati jadidifu, kulingana na malengo ya taifa na kimataifa.
Aidsha
Megawati 50 zitakazozalishwa zitaongeza kiasi cha umeme kinachosambazwa
kwenye Gridi ya Taifa, na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa wananchi,
viwanda, na biashara kwa bei nafuu.
Mradi huu wa Shinyanga unajumuisha dhana pana ya
utekelezaji wa miradi mikubwa nchini, ambayo wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wanaitaja kama "Huyu Ndo Mama Samia Sasa."
Kasi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo imeongezeka, ikiwemo:
• Miundombinu:
Ujenzi wa barabara, mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) Mbagala, na miradi
mingine ya kimkakati.
• Huduma
za Jamii: Kuongeza miradi ya umeme vijijini (REA), na uwekezaji mkubwa katika
ujenzi wa shule, vituo vya afya, na hospitali nchini.
• Sekta
ya Elimu: Kufanya mabadiliko katika mfumo wa elimu kwa kuweka mtaala wa amali
(ujuzi), unaowawezesha vijana kujitegemea, sambamba na uwekezaji katika
miundombinu ya ufundishaji.
• Uongozi,
Amani, na Umoja: Kuendelea kuiongoza nchi vizuri, kuhakikisha amani na umoja
vinadumu, na nchi inakuwa katika mikono salama kuelekea kipindi cha uchaguzi.
Kukamilika kwa mradi wa umeme wa jua Shinyanga
kunatoa ishara thabiti ya mwelekeo wa nchi katika kuimarisha miundombinu ya
kiuchumi na kuleta ustawi kwa wananchi, huku Mkoa wa Shinyanga ukianza kuang’aa
kwa nguvu ya jua, ikiashiria nguvu ya maendeleo.

0 Maoni