Tanzania
kupitia Viongozi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum imeshiriki katika Mkutano wa Viongozi wa Dunia Kuhusu Wanawake
“Global Leaders' Meeting on Women” uliofanyika Beijing, nchini China.
Akizungumza jana kando ya Mkutano huo Msajili wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Vickness Mayao ambaye ni Kiongozi wa ujumbe wa
Tanzania amesema wameshiriki Mkutano huo kwa lengo la kujifunza na kutoa uzoefu
wa namna bora ya kufikia Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa wanawake.
"Tumejadili
mafanikio na changamoto zinazokabili nchi mbalimbali katika kufikia usawa wa
kijinsia na uwezeshaji wanawake tangu kuwekwa kwa maazimio ya malengo ya
Beijing mwaka 1995" amesema Vickness
Naye
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Wanawake kutoka Wizara hiyo Juliana Kibonde
amesema mkutano ulioandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu China chini ya
Umoja wa Wanawake wa Chama Tawala “All-China Women’s Federation” kwa
kushirikiana na U.N Women umekuwa na mchango mkubwa hasa kwa nchi mbalimbali
kujifunza na kueleza mafaniko na changamoto zao katika kufikia Usawa wa
Kijinsia katika Mataifa yao.
"Mkutano
ulikuwa na lengo la kusherehekea na kufanya tathmini ya miaka 30 ya Mkutano wa
Beijing uliofanyika mwaka 1995 hapa Beijing na sasa ni miaka 30 tukiwa
tunasherekea mafanikio ya utekelezaji wa malengo 12 ya Mkutano huo ambayo kila
nchi ilichagua kutekeleza na kuangalia changamoto zilizobaki ili kuweza kutatua
na kuzifanyia kazi ili kuwa na Dunia yenye Usawa wa jinsia na Uwezeshaji wa
wanawake," amesisitiza Juliana.
Mkutano
huo ulifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping huku
ukihudhuliwa na Viongozi wakuu wa nchi na Serikali, Mawaziri pamoja na Mabalozi
kutoka takribani nchi zaidi 110, Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mashirika
mbalimbali ya Kimataifa huku zaidi ya washiriki 800 wakihudhuria mkutano huo.
Mkutano
huo uliongozwa na kaulimbiu isemayo "Mustakabali wa Pamoja: Mchakato Mpya
na Uliorahishwa kwa Maendeleo Jumuishi ya Wanawake".


0 Maoni