Mgombea
wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Chama cha Ukombozi
wa Umma (CHAUMMA) Salim Mwalimu amesema kwamba hatomuacha Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa iwapo atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi mkuu Oktoba 2025.
Malimu
ametoa kauli hiyo jana akiwa mkoani Lindi, katika mwendelezo wa kampeni za
chama hicho, ambapo ameahidi kutoaacha uzoefu wa miaka 10 ya Uwaziri Mkuu wa Mhe.
Majaliwa upotee hivi hivi.
“Mimi
nawaahidi kuwa sitamuaacha Mhe. Majaliwa katika serikali yangu nitakayoiunda
mtakapo nichagua, nitafanya kazi na majali atapata nafasi yake ili aendelee kutupatia
uzoefu wake,” alisema Mwalimu.
Amesema
kwamba yeye hatoingia Ikulu kufukua makaburi, wala hana mpango wa kuwahukumu
watu bali atafanya maridhiano ya kitaifa na kuwasamehe wale wote waliofanya
makosa wakiwa madarakani.
“Nawaahidi
serikali yangu kamwe haitaenda kulipa kisasi wala kumuhukumu mtu, sisi sote ni
wanadamu na mwanadamu ameumba wakiwa na uwezo wa kufanya makosa, hivyo mimi si
Mungu niwahukumu,” alisema Mwalimu.
Amesema
kwamba hata Jeshi la Polisi hatofanya mabadiliko ataendelea na hao hao akiwamo Mkuu
wa Jeshi la Polisi IGP Camillius Wambura, “Nitaendelea na IGP Wambura simfukuzi
kazi labda ajitekenye mwenywe (akosee) mimi nifanyaje sasa ?,” alisema Mwalimu.

0 Maoni