Salamu
nyingi za shukrani natoa kwenu wana Mbeya, mikoa ya jirani na wote mliotoa muda
wenu kuhudhuria sherehe za kilele za Mbio za Mwenge wa Uhuru. Na kubwa zaidi ni
Uzinduzi wa Kitabu cha kumbukumbu ya Miaka 60 ya Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa
Uhuru 2025 umeacha historia kubwa sana. Ukiacha umbali uliokimbia na idadi ya
miradi iliyokaguliwa na thamani yake ni wazi kuwa Mbio za Mwenge mwaka huu
zimeacha historia katika masikio na macho yetu kutokana na ukweli kuwa sherehe
zimepambwa vzr na halaiki ya safari hii ilikuwa ya kipekee na yenye kusisimua.
Hii
inatokana na ainaya watu walioshiriki ambapo kwa mara ya kwanza Watoto wenye
Ulemavu wa viungo nao pia wameshiriki. Ni jambo ambalo halijawahi tokea.
Kama
ilivyoada Kilele uanza na misa takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa , Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere. Tunalishukuru Kanisa katoliki kwa kuongoza misa hiyo
kwa mafanikio makubwa. Tuzidi kumuombea Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere.
Mgeni
Rasmi Dk. Philip Mpango , Makamu wa Rais Wa JMT alifunga maonyesho ya kazi za
vijana yaliyofanyika kwa siku 7 katika eneo la uhindini hapo hapo Mbeya.
Maonyesho haya yalionyesha vipaji mbalimbali vya vijana na ubunifu. Nayo
yameacha kumbukumbu nzuri kwa idadi ya washiriki na kazi walizoshiriki. Kwa
hakika imefana sana.
Mwenge wa
Uhuru 2026 unataraji kuwashwa Mkoa wa Kusini
Pemba na baada ya kuzungushwa Nchi nzima utafikia kilele Mkoani Rukwa
ambapo pia tutafanya Maonyesho ya kazi za Vijana katika wiki ya vijana, pamoja
na kongamano kubwa la Vijana.
Ninarudia
kuwashukuru sana Wanambeya kwa ushiriki na utayari wao. Kipindi chote
umeonyesha utayari kwa kuhudhuria kwa wingi
wiki ya maonyesho ya kazi za vijana. Kila siku makundi kwa makundi;
ushiriki wenu kwenye Kongamano la Vijana na uwazi wetu katika kujadili na wisho
ushiriki wenu kwenye misa. Tunawashukuru sana. Kwa hakika wameuenzi Mwenge wa
Uhuru ambao umeendelea kuwa moja ya Tunu katika Umoja wa Nchi yetu.
Asanteni
Mbeya
#MwengeWaUhuru2025



0 Maoni