Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
akionesha Tuzo ya Presidential Global Water Changemakers 2025 ambayo
alitunukiwa tarehe 13 Agosti, 2025 Cape Town, nchini Afrika Kusini.
Tuzo
hiyo iliwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 26 Oktoba,
2025.
Tuzo
hiyo ya Ulimwengu ya Marais wanaoleta Mabadiliko katika Sekta ya Maji imetolewa
kwa kutambua uongozi bora na dhamira ya dhati katika kuanzisha na kuendeleza
mipango na miradi ya Maendeleo katika Sekta ya maji nchini Tanzania.

0 Maoni