Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2025 amewasili Seychelles kwa ajili ya
kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais mteule wa
sita wa nchi hiyo Dr. Patrick Herminie.
Tume
ya Uchaguzi ya Taifa ilimtangaza Mheshimiwa Dkt. Patrick Herminie wa Chama cha
United Seychelles (US) kuwa mshindi baada ya kumbwaga Rais aliyekuwa
madarakani, Mheshimiwa Wavel Ramkalawan wa Chama cha Linyon Demokratik Seselwa
(LDS).
Mheshimiwa
Dkt. Patrick Herminie alipata asilimia 52.7% ya kura, huku Rais Wavel
Ramkalawan akimaliza wa pili kwa kupata 47.3% ya kura.



0 Maoni