Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameidhinisha Oktoba 29, 2025 kuwa siku ya mapumziko ili
kuwawezesha Wananchi kupiga kura, kwa kutumia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria
ya Sikukuu za Kitaifa sura ya 35, taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imesema.
“Kama
inavyofahamika, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza siku ya
Jumatano tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku ya kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi
wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025,” imesema taarifa hiyo na kuongeza “uamuzi
huo wa Rais umekuja kwa madhumuni ya kuwawezesha Wananchi wenye sifa stahiki
wakiwemo Watumishi wa Umma na Wafanyakazi katika Sekta Binafsi kutumia haki yao
ya kikatiba ya kupiga kura,” imeeleza taarifa hiyo.


0 Maoni