Mange Kimambi, mfanyabiashara wa mitandao anayeishi
Marekani, kazi yake kuu ni kuchochea fujo ili apate content (naudhui) ya kuuzia
wafuasi wake na kujikusanyia mabilioni ya shilingi. Ndoto yake ya kuona vurugu
na fujo zikilipuka Tanzania inabaki kuwa biashara ya kutengeneza maudhui ya
uongo na kuzua mtafaruku.
Wiki hii, Mange ameonekana tena akitoa maelekezo kwa
vijana na wanajeshi wa Tanzania kuhusu mpango wake wa kuichafua nchi. Hata
hivyo, mara hii, sauti yake ilikuwa ilijaa shaka, akionesha woga wa
kutofanikiwa kwa mpango huo wa kibiashara.
Ukweli wa Biashara Yake:
Mange anafanya biashara ya maudhui yenye misingi ya
chuki, matusi, na fedheha dhidi ya viongozi, wasanii, na wanasiasa. Biashara
hii inamuingizia zaidi ya Shilingi Bilioni 1.5 kwa mwezi, huku kila subscriber
akilipa takribani Shilingi 1,500. Huu ndio msingi wa uchochezi wake, si ajenda
ya kizalendo.
Vijana Waendelee Kumpuuza:
Maandamano aliyoyapanga Marekani, katika Ubalozi wa
Tanzania Washington DC, yalihudhuriwa na watu wasiozidi kumi. Hii ilithibitisha
kwamba vijana wa Tanzania wamepuuza na kutambua udanganyifu wake. Licha ya
Watanzania zaidi ya 100,000 kuishi Marekani, hakuweza kukusanya hata asilimia
ndogo sana!
Uoga wa 'Mwanaharakati': Mange mwenyewe hakuthubutu
kujitokeza, akidai jeshi la Marekani limemwonya. Je, huu ndiyo ujasiri wa
kiongozi anayedai anaongoza kizazi cha mabadiliko? Vijana, mpuzeni kiongozi
mwenye woga anayetaka kuwahatarisha wengine.
Tanzania Ni Nchi Ya Kazi, Siyo Ya Kelele: Wakati
Mange anataka machafuko, vijana wa Tanzania wako kazini, wanasomea taaluma,
wanabuni biashara, na kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwamo kilimo na
utalii. Katika kilimo mashamba ya umwagiliaji yameongezeka kutoka hekta 540,000
(2021) hadi zaidi ya milioni moja (2024).
Pia pato la taifa kutoka utalii limeongezeka, na
vijana wako Zanzibar, Arusha, na Kilimanjaro wakihudumia watalii zaidi ya
Milioni 5.3!
Tanzania ni Taifa lenye amani, matumaini, na kazi.
Uchochezi wa Mange Kimambi utabaki hewani kama matangazo ya mtandaoni yasiyo na
tija. Vijana, endeleeni kulinda amani, fanyeni kazi, na msimpe
"content" ya fujo anayoitaka.

0 Maoni