WAZIRI wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani
Kikwete amefika mkoani Mbeya kukagua na kutazama maandalizi ya sherehe za
Kuhitimisha Mbio za Mwenge wa uhuru zitakazotanguliwa na Maonyesho ya kazi
Mbalimbali na huduma katika Wiki ya Vijana na Kongamano kubwa litakalokutanisha
vijana zaidi ya 1500, sinazotaraji kufanyika mjini Mbeya.
Maonyesho ya Wiki ya Vijana yameanza 8 Oktoba na
kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba 2025 pamoja na Kongamano la Vijana ambalo mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano Wa Tanzania.
Shughuli zote zitahitimishwa na sherehe za kilele
cha Mwenge wa Uhuru 2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Dr. Samia Suluhu
Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika ziara hiyo Ridhiwani amepata nafasi ya
Kukagua matayarisho ya shughuli hizo zote na kukutana na wananchi, kuwasalimia
na kuwakaribisha kuja kushiriki shughuli hizo zote.
"Karibuni sana Mbeya, tusikilize Nini Mwenge wa
Uhuru Umeona," alisema Kikwete.
0 Maoni