Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Felister Mdemu amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya kufanya kazi
kwa bidii na kujituma katika kuwahudumia wananchi katika vituo vyao vya kazi.
Mdemu
ameyasema hayo jana, wakati akikabidhi Pikipiki kumi na mbili (12) kwa Maafisa
Maendeleo ya Jamii katika hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya lengo kuu ikiwa ni kuwasaidia Maafisa hao hasa wanaoishi vijijini
kuzitumia kuwafikia wananchi na kuwahudumia kwa wakati.
Mdemu
amesema lengo kuu la kuwapatia pikipiki hizo ni kutambua thamani ya mchango wao
kiutendaji pamoja na kuwarahisishia kazi wakati wa ufuatiliaji na utatuzi wa
changamoto za kijamii.
"Tunaomba
mkawajibike ipasavyo kwani kwa sasa mmerahisishiwa utendaji kazi wenu kwa
kupewa vyombo vya usafiri (Pikipiki) ili kuwafikia wananchi katika maeneo yao
na kuwahudumia." amesema Mdemu.
Naye
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Anna Mwambene ameishukuru Wizara kwa
kuwapatia Maafisa hao vyombo vya usafiri hivyo ambavyo anaamini vitaleta chachu
na mabadiliko katika kuwahudumia wananchi mkoani humo.
"Mmekabidhiwa
pikipiki hizi mzitunze ili zifanye kazi ilivyokusudiwa na niiombe Wizara kuendelea
kusaidia vyombo vya usafiri kila wakati ili kukidhi mahitaji ya Maafisa
Maendeleo ambao kazi zao zinawahitaji kusafiri umbali mrefu kuwafuata wananchi
walipo." amesema Anna.
Aidha
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya Elukaga Mwaikasu amewataka Maafisa
Maendeleo ya Jamii Kata waliopewa vyombo vya usafiri (pikipiki) hivyo
kuhakikisha wanavitunza na kwa yeyote atakayeharibu makusudi au kukitumia
chombo ndivyo sivyo hatua za kisheria zitachuliwa dhidi yake.
Kwa
upande wao Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata waliopokea vyombo vya usafiri
(pikipiki) hivyo wameipongeza Serikali kwa kutoa vitendea kazi na kuahidi
kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuwatumikia na kuwahudumia wananchi kwa weledi
na kwa ufanisi.


0 Maoni