Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, wananchi wanahimizwa kutumia haki yao ya kidemokrasia.
Kauli ya "Kura
yako ni sauti ya amani, daraja la maendeleo, na mwanga wa kesho bora"
inawahimiza Watanzania "watoke" Oktoba hii, kwenda kupiga kura kama
haki yao ya msingi.
Mfanyabiashara wa
soko la Chifu Kingalu Morogoro Yusuf Hamad Brush anasema kwamba ni vyema watu
wakatoka katika majengo yao na maeneo ya kazi kwenda kupiga kura Oktoba 29 kwa
sababu hiyo ndio maana ya maendeleo.
Anasema usipoenda
kupiga kura utakuwa unajimnyima maendeleo yako mwenyewe na hasa uchaguzi wa mtu
kukuwezesha kuwa na maendeleo unayoyataka.
Anasema uchaguzi ndio
njia pekee ya kupanga maendeleo na Amani ya taifa.
Anasema yeye mwenyewe
ataoenda kupiga kura kwa kuwa anaamini kwamba kura hiyo ndio msingi wa
mabadiliko anayoyataka nchini.
Katika kuhimiza
upigaji kura, rekodi ya mgombea Dkt. Samia Suluhu Hassan inatumiwa kama
kielelezo cha maendeleo endelevu ya Taifa. Serikali yake imejikita katika
kubadilisha taswira ya miundombinu nchini, jambo linalochukuliwa kama msingi wa
kuendeleza uchumi na urahisi wa maisha.
Katika Sekta ya
Usafiri na Miundombinu:
Utekelezaji wa miradi
mikubwa unatajwa, ikiwemo kukamilisha ujenzi wa barabara ya juu ya Ubungo na
kuanzisha mipango ya barabara za juu mikoani. Kazi kubwa inaendelea katika
ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, hatua muhimu
itakayobadilisha usafiri nchini.
Dkt. Samia pia
anatajwa kusimamia ujenzi wa madaraja makubwa kama Daraja la Kigongo–Busisi na
Daraja la JPM, ambayo yanajenga daraja la maendeleo kwa kuunganisha mikoa kwa
urahisi zaidi wa kibiashara na kijamii.
Aidha, juhudi
zimefanywa kuboresha viwanja vya ndege vya kisasa katika mikoa muhimu kama
Dodoma, Mwanza, na Kigoma, huku mfumo wa usafiri wa mwendokasi (DART) jijini
Dar es Salaam ukiwa umeboreshwa kwa kuongeza njia mpya na magari ya kisasa.
Mbali na miundombinu
ya usafiri, Dkt. Samia pia ametajwa kufanikisha ujenzi wa nyumba bora za watumishi
wa umma kote nchini.
Wito unaendelea
kutolewa kwa wapiga kura kutumia kura yao "kwa Samia" mnamo Oktoba,
wakisisitiza kauli mbiu ya "Kazi na utu tunasonga mbele."

0 Maoni