Idara ya
famasia kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila imepatiwa mafunzo
kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuhusu dawa zisizo na ubora, dawa
bandia na dawa zisizosajiliwa ili kuendelea kutoa huduma bora za dawa kwa
wagonjwa.
Akitoa
mafunzo hayo mtoa mada kutoka TMDA mfamasia na mkaguzi Keddy Manga amesema
wafamasia wanatakiwa kuzingatia ubora, usalama na ufanisi wa dawa wanazopokea
na kuzitoa kwa wagonjwa.
Mafunzo
hayo yametolewa kwa lengo la kuwasaidia
wafamasia wa hospitali kubaini dawa ambazo hazijasajiliwa nchini(unregistered),
dawa na vifaa tiba visivyo na ubora (substandard) , dawa na vifaa tiba bandia (counterfeits)
pamoja na kuangalia rangi ya dawa na maandishi ya lebo.


0 Maoni