Serikali Ya Awamu Ya Sita Yaweka Msingi Imara Kwa Wasichana
Tukiwa tunaelekea
katika Uchaguzi, ni muhimu kutambua kwamba maendeleo ya taifa letu yanategemea
amani na utulivu. Taifa linahitaji vijana wanaojua Sayansi, na hii inawezekana
tu katika mazingira ya utulivu, ambapo masomo yanaendelea vizuri.
Serikali ya Awamu ya
Sita imejitosa kikamilifu kuhakikisha watoto wa kike wanachomoza katika masomo
ya Sayansi kwa vitendo. Utekelezaji wa ujenzi wa Shule 26 za Sekondari za
Wasichana za Sayansi (Shule moja kwa kila Mkoa wa Tanzania Bara) ni ushahidi wa
azma hii.
Shule ya Sekondari ya
Wasichana Shinyanga ni mfano mmoja wa shule hizi ambazo zimejengwa mahususi kwa
lengo la kuwawezesha watoto wa kike kufundishwa Sayansi kwa ubora, na hivyo
kuongeza idadi ya Wanasayansi nchini.
Jumla ya Shilingi
155,240,120,476.81 zimetumika katika miradi hii ya maendeleo ya elimu.
Ubora wa shule hizi
unazdhirisha na utimilifu wake kama
wanafunzi hawa wanavyotumia maabara za kisasa (kwenye picha). Lakini maendeleo
haya yataendelea na kuwa na maana kama tu tukiilinda amani.
Mwanafunzi Mmoja
Aliyefaidika wa shule ya Shinyanga alisema:"Ninamshukuru sana Rais wetu
kwa kuwajali wasichana. Miradi hii imetusaidia sana kwa kutuondolea vishawishi
na kutupatia mazingira bora ya kupata elimu bora. Tumeona kwamba wasichana
tukipewa nafasi, tunaweza kufanya makubwa katika Sayansi kama watoto wa
kiume!"

0 Maoni