
Kamishna wa Uhifadhi wa mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro Bw. Abdul-Razaq Badru amefanya ziara katika eneo la Ndutu lililopo
hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kukagua ukarabati wa Miundomninu ya utalii
kuelekea msimu wa utalii katika eneo hilo ambalo ni maarufu kwa mazalia ya
Nyumbu wanaohama.
Akiwa katika eneo hilo Kamishna Badru amekagua mradi
wa ujenzi wa tenki la Maji lenye mnara wa mita 6 ambalo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi
lita 50,000 za maji kwa ajili ya matumizi ya wageni wanaotembelea eneo hilo,
maafisa na askari waliopo kanda ya Ndutu sambamba na hoteli na kambi za kulala
wageni zilizopo Ndutu.
Aidha, Kamishna Badru akiwa katika eneo hilo
Kamishna Badru amesema Ngorongoro itaendelea kuboreshea mazingira ya uwanja wa
ndege wa Ndutu ili kuwa rafiki kwa ndege zinazoleta wageni katika eneo hilo
ambapo msimu wa kuzaa na kuhama kwa Nyumbu mwezi Desemba hadi Machi ndege ndogo
15 hadi 20 hutua kila siku katika eneo hilo kuleta wageni
Katika ziara hiyo Badru amezungumza na askari wa
jeshi la uhifadhi katika kanda ya ndutu kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya
ulinzi na uhifadhi katika eneo hilo ikiwemo kuimarsisha usalama wa wageni na
mali zao pamoja na rasilimali za Wanyamapori na Misitu.




0 Maoni