Jeshi la
Polisi nchini limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni
zinazomhusu Ndugu Godbless Lema anayedai kwamba usalama wa maisha yake upo
hatarini.
Ufafanuzi
huo unakuja kufuatia maombi kutoka kwa Waandishi wa Habari kuhusu suala hilo.
Msemaji
wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi, Dodoma, amesema Jeshi hilo
linaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa hiyo.
Hata
hivyo, Jeshi la Polisi limemsisitiza Ndugu Lema afike katika Kituo cha Polisi
ili aweze kuwasilisha taarifa yake hiyo rasmi na kwa njia zinazokubalika
kisheria. Uwasilishaji wa taarifa rasmi utawezesha Jeshi la Polisi kuchukua
hatua stahiki kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
Aidha,
Jeshi la Polisi limetoa wito na kusisitiza kwa baadhi ya viongozi wa wananchi
kuendelea kuzingatia utaratibu wa kisheria wa kuwasilisha taarifa sahihi kwa
mamlaka za Haki Jinai.
Lengo la
wito huo ni kuepusha upotoshaji na taharuki zisizo za lazima ambazo huweza
kusababishwa na taarifa zisizothibitishwa au kuwasilishwa katika maeneo yasiyo
rasmi.
Taarifa
hiyo iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesisitiza umuhimu wa kufuata utaratibu na
sheria wakati wote.

0 Maoni