Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imewalipa Shilingi bilioni 1.6 wananchi 213 wa Kijiji cha Mpeta Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, wanaopisha utekelezaji wa mradi wa SGR kipande cha sita Tabora hadi Kigoma.
Hassan
Mbaga ambaye ni mthamini na msimamizi wa zoezi la ulipaji fidia kutoka Shirika
la Reli Tanzania (TRC) amesema mradi wa SGR ni wa usanifu na ujenzi hivyo
maeneo yanayohitajika kwa shughuli za mradi yamekuwa yakichukuliwa kwa hatua,
hivyo kufanya zoezi la ulipaji fidia kuwa endelevu.
Hassan
Mbaga ambaye ni ni mthamini na msimamizi wa zoezi la ulipaji fidia kutoka
Shirirka la Reli Tanzania (TRC) amesema katika awamu ya pili ya ulipaji fidia
katika kipande cha sita Tabora hadi Kigoma Serikali imelipa Shilingi bilioni
1.6 kwa wananchi 213 wa Kijiji cha Mpeta wilayani uvinza Mkoani Kigoma.
Akizungumzia
zoezi hilo, Katibu Tarafa wa kata ya Nguruka, Wilaya ya Uvinza, Bwana Lyola
Proches, ambaye katika zoezi la ulipaji fidia alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya
Uvinza Mhe. Dinah Mathaman, alitoa wito
kwa wananchi waliopokea fidia husika kuzitumia fedha walizopokea kwa
umakini ambapo alisema, ‘’natoa rai kwenu kwamba fedha mlizopokea mkazifanyie
malengo yaliyo sahihi hususani kurudisha vile vipande vilivyotwaliwa badala ya
kufanya matumizo yasiyo na tija’’, alisisitiza Katibu Tarafa wa kata ya
Nguruka, Wilaya ya Uvinza, Bw. Lyola Proches.
Wakati
huo huo mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mpeta Bw. Lifa Hamad Alpha, kwa niaba
ya wenzake waliopokea fidia husika, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa
kutekeleza ile ahadi waliyopewa kwenye fidia na kurudisha Maghala ya kuifadhia
mpunga hivyo kuendelea na shughuli za kilimo.
Katika
hatua nyingine, afisa Jamii kutoka Shirika la Reli TRC Lucy Maroda amesema
Elimu waliyoitoa katika ulipaji Fidia itakwenda kuwasaidia wananchi hao ili
kutimiza malengo yao na kufanya Uchumi wa wananchi kuimarika.


0 Maoni