Mgombea
Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi bado yupo
mkoani Tabora ambako anaendelea na kampeni za kunadi sera za chama hicho pamoja
na kuomba kura kuelekea Uchagzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
Dk.Nchimbi
katika kampeni hizo anaendelea kuipeperusha bendera ya chama hicho akinadi sera
na kuwanadi wagombea katika maeneo yote anayopita akiwemo Mgombea Urais wa CCM
Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa
mujibu wa ratiba ya kampeni hizo, Dkt. Nchimbi leo Oktoba 05, 2025 atafanya
mikutano miwili ambapo ataanza na mkutano Sikonge kwenye Uwanja wa TASAF na
kisha atamaliza siku yake kwa mkutano mkubwa utakaofanyika Kaliua kwenye
Viwanja vya Konane.


0 Maoni