Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 17
Oktoba 2025 amewasili Nairobi nchini Kenya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mazishi ya
Kitaifa ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya marehemu Raila Amolo Odinga.
Mazishi
ya Kitaifa ya marehemu Raila Odinga yanatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa
Nyayo Jijini Nairobi.
Makamu wa
Rais ameambatana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo.



0 Maoni