Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt. Doto Mashaka
Biteko amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono na maelekezo yaliyowezesha
utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wilayani, mkoani na Taifa kwa
ujumla.
Dkt. Doto
Biteko amesema hayo mbele ya Mgombea Urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan akiwa katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika Wilaya ya Bukombe,
ikiwa ni sehemu ya Kampeni zake Mkoani Geita Oktoba 12, 2025.
“ Mgombea
umetufundisha mengi, kupitia kauli mbiu yako ya kazi na utu tunasonga mbele,
unatenda zaidi na kusema kidogo. wewe unazungumza matatizo ya watu na maisha
yao wakati wote, Utu kwako ni kipaumbele na Kazi kwako ni msingi wa maendeleo”
amesema Dkt. Biteko.
Ametaja
miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ikiwemo
Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, Daraja la JPM, Barabara za lami ndani
na nje ya Wilaya ya Bukombe pamoja na taa za barabarani ili kuweka mazingira
bora ya ufanyaji wa Biashara.
Dkt.
Biteko pia amemshukuru Dkt. Samia na kuahidi kuendelea kuwa msikivu, mwaminifu
mwadilifu ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji katika nafasi yake ya usaidizi.




0 Maoni