Kila mara
tunapokaribia uchaguzi, mijadala hujawa na mbwembwe, matusi na maneno matupu
yanayopoteza muda. Lakini Uongozi wa kweli sio makelele jukwaani; ni uwezo wa
kutafsiri maono makubwa kuwa matendo halisi yanayoleta maendeleo na fursa za
ajira kwa wananchi.
Huu ndio
wakati wa kuingia kwenye sanduku la kura kuamua mabadiliko kwa kutambua
kiongozi anayesema ukweli unaogusa mahitaji yetu ya msingi na anayeweza
kusimamia mabadiliko yaliyokusudiwa.
Kiukweli,
kura yako ni muhimu sana kwani inatoa mamlaka ya kusimamia mabadiliko makubwa
ya Taifa hili. Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania inaendelea kuandika
historia mpya ya maendeleo kupitia miradi mikubwa ya usafiri wa kisasa na kazi
hii inahitaji usimamizi wa karibu.
Baada ya
mafanikio makubwa ya Reli ya Kisasa (SGR) inayotumia umeme, sasa macho ya
Watanzania yanaelekezwa kwenye hatua nyingine kubwa zaidi ya kuboresha
miundombinu ya usafiri.
Mtaalamu wa
Miundombinu, Bw Salum Mturi, anasisitiza: "Kama hatutapiga kura kwa
kiongozi mwenye maono ya miundombinu, tutabaki kwenye foleni kwa miaka mingine
mitano. Kura yetu ndiyo inahakikisha Serikali inaendelea na kasi hii."
Chini ya
uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mpango uko tayari wa kuanza ujenzi wa
treni za mijini (Metro) katika majiji ya Dar es Salaam na Dodoma katika kipindi
cha miaka mitano ijayo. Mradi huu ni sehemu ya mpango mpana wa kuboresha maisha
ya wananchi kwa kupunguza msongamano, kurahisisha usafiri, na muhimu zaidi,
kukuza uchumi wa mijini.
Wakati Dar es
Salaam inajiandaa kuwa “megacity” ya kwanza Afrika Mashariki yenye wakazi zaidi
ya milioni 10, Mradi wa Metro na ujenzi wa miundombinu inayouzunguka
unahakikisha ukuaji huu wa watu unakwenda sambamba na ufanisi wa usafiri. Huu
si tu ujenzi wa miundombinu; ni injini ya kutoa ajira kulingana na mahitaji
yetu halisi.
Maeneo kama
Morocco, Mwenge, Magomeni na Tabata yanatarajiwa kupata barabara za juu
(flyovers), ambayo yanatarajiwa kujengwa barabara hizo yanamaanisha kazi nyingi
za ujenzi, uhandisi, na usimamizi.
Bi. Neema
John, mhitimu wa Uhandisi (25), anasema: "Miradi mikubwa kama flyovers na
Metro inamaanisha ajira kwetu. Mimi sitapiga kura kwa maneno matupu, nitapiga
kura kwa yule anayeonesha wazi mahali pa kwenda kufanya kazi."
Kila mradi
unaotekelezwa, ukiwemo wa Arena (ukumbi mpya wa kimataifa utakaobeba watu
15,000) katika eneo la Kawe, unatafsiriwa kuwa fursa mpya za ajira ndogondogo
na uwekezaji katika sekta binafsi.
Kama
ilivyokuwa ndoto kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa saa moja
kupitia SGR, sasa treni za Metro zitakuwa ishara ya zama mpya za ufanisi na
teknolojia. Huu ndio ukweli tunaokubaliana nao kama mahitaji yetu.
Acha Mbwembwe
Wakati wa
kupiga kura, acha kupoteza muda na mbwembwe na badala yake, angalia matokeo ya
kazi. Kura yako lazima iwe kwa dira ya maendeleo, kasi, na uthubutu ambayo
inajibu moja kwa moja mahitaji ya ajira na maisha bora ya mwananchi.

0 Maoni