Takriban watu 17 wamethibitishwa kupoteza maisha baada ya kiberenge cha waya aina ya funicular ya Gloria, maarufu kwa watalii, kuacha reli na kugonga jengo katika jiji kuu la Lisbon, Ureno.
Taarifa za mamlaka zinasema zaidi ya watu 20 wamejeruhiwa, wakiwemo raia wanne wa Ureno, wawili kutoka Ujerumani na wawili kutoka Hispania. Mtoto wa miaka mitatu pia ameripotiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo mbaya.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa linashirikiana kwa karibu na kampuni inayoendesha kiberenge hicho maarufu kwa watalii ili kubaini idadi kamili ya watu waliokuwemo ndani wakati wa ajali pamoja na chanzo halisi cha tukio hilo.
Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zinaeleza kuwa moja ya nyaya za kiberenge hicho ilikatika wakati kikiwa katika mwendo, jambo lililosababisha dereva kupoteza udhibiti na hivyo kusababisha ajali hiyo mbaya.
Serikali ya Ureno imetangaza siku ya maombolezo ya kitaifa huku juhudi za uokoaji na uchunguzi zikiendelea katika eneo la tukio.
0 Maoni