MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara
Stephen Wasira amesema kwamba kazi ya chama hicho kwa sasa ni kuisaka dola
kwani mchakato wa kura za maoni zilishapita hivyo hakuna sababu ya kuwa na
mgawanyiko tena.
Wsira ameyasema hayo Agosti 31,2025 alipokuwa akizungumza na
viongozi wa Chama hicho wakati wa kikao cha ndani ambapo ametumia kikao hicho
kuelezea mchakato wa kura za maoni hadi kupatikana walioteuliwa kugombea ubunge
na udiwani.
"Kazi yetu ni kuhakikisha mtu ashinde... kwahiyo muache
kugawanyika kwasababu kura za maoni zimeshapita hivyo tugawanyike kwa ajili ya
zile.
"Wewe unagombana na hewa maana kura zile zimeshapigwa,
tena unagombana na mtokeo ambayo na wewe mwenyewe ulikuwepo wakati wa kuhesabu
kura umeshuhudia halafu unamkasirikia nani? Unakasirikia matokeo au
aliyetangaza, unamkasirikia nani?, alihoji Wasira.
"Hakuna hoja hapo bali kwa sasa hoja ni CCM kupata dola
na hayo mengine yote tunayoyafanya yote ni mchakato wa kufikia lengo la kupata
dola.Hivyo msipoteze lengo kwasababu ya mchakato wa ndani, huo ujumbe wangu wa
leo,"amesem Wasira.
Amefafanua uongozi huo na kazi ya kusema nani anakuwa na
nani hawi ni kazi mbaya na ngumu na amewaambia kutokana na nguvu ya ubinadamu
maana wao sio malaika na mpaka hapo walipofikia ni vema wakapongezwa maana kazi
yenyewe ngumu.
"Nilikuwa namwambia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha
rafiki Sabaya mbona mwanao hakuteuliwa ,nami nilikuwa na mwanangu anagombea
lakini hakuteuliwa na mimi ndio Makamu Mwenyekiti.
"Sasa wewe unanung'unikia nini? Ni kazi ngumu lakini
nataka niwaambie walioteuliwa sio kwamba wao ni bora kuliko wasioteuliwa, sio
kweli ila hili chama lina watu wengi halafu wanauwezo.Hata ukiondoa
walioteuliwa ukaamua kupata wwngine tena watakuja wengi na wenye uwezo zaidi ya
hawa."
0 Maoni