Maporomoko
ya ardhi yameua watu wapatao 1,000 katika eneo la mbali la Milima ya Marra,
magharibi mwa Sudan, kwa mujibu wa kundi la waasi la Jeshi la Ukombozi wa Sudan
(Sudan Liberation Movement Army).
Mvua kubwa
zilizonyesha kwa siku kadhaa zilisababisha maporomoko hayo siku ya Jumapili, na
kundi hilo limesema katika taarifa kuwa mtu mmoja tu ndiye aliyenusurika na
kuwa kijiji cha Tarasin "kimesawazishwa kabisa".
Kundi hilo
limeomba msaada wa kibinadamu kutoka kwa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine
ya kikanda na kimataifa.
Wakazi wengi
wa jimbo la Darfur Kaskazini walikimbilia eneo la Milima ya Marra kutafuta
hifadhi, baada ya vita kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha
Rapid Support Forces (RSF) kupelekea kuzikimbia nyumba zao.
0 Maoni