Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Makunduchi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Wanu
Hafidh Ameir akiwa katika Viwanja vya Jamhuri vilivyopo Makunduchi, Kusini
Unguja jana tarehe 26 Septemba, 2025 amenadi Sera zake kwa kwa Wanamakunduchi na
kuomba ridhaa kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba,
2025 nchi nzima.
Aidha,
Mgombea Ubunge Jimbo la Makunduchi, Wanu Hafidhi Ameir amehutubia wananchi na
kuweka bayana vipaumbele kadhaa ikiwemo;
Kwanza;
Kujenga ukuta wa Hospitali ya Wilaya Makunduchi
Pili;
Kuwawezesha kifedha Wanawake wakulima wa zao la Mwani
Tatu;
Kuwanunulia Gari Wanawake Wakulima wa
zao la Mwani ambalo watalitumia kwenye shughuli zao za Mwani
Vilevile,
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Makunduchi, Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman kwenye
mkutano wa kampeni za CCM pamoja na wagombea wengine wamenadi sera zao kwa
wananchi na kuomba kura ili kupata ridhaa ya kuchaguliwa kuelekea Uchaguzi Mkuu
wa Oktoba 29, 2025.
Pamoja na
mambo mengine, Wanu Hafidh Ameir amewaomba wana Makunduchi wote kumpigia kura
Mgombea Urais Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan; Mgombea Urais Zanzibar, Dkt.
Hussein Ali Mwinyi; Mgombea Ubunge Makunduchi; Mgombea Uwakilishi Makunduchi na
Madiwani wa Wadi za Makunduchi.
#MakunduchiMpya
#MakunduchiNiYetu
#OktobaTunatiki
#KaziNaUtu
#TunasongaMbele

0 Maoni