Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amewakaribisha Sekta
Binafsi kuwekeza katika maeneo ya Hifadhi Nchini, ikiwemo Hifadhi ya Swagaswaga
ambayo ni kitovu cha utalii katika Jiji la Dodoma.
Dkt.
Abbasi aliyasema hayo, Septemba 26,2025, alipofanya ziara ya kikazi katika
Hifadhi ya Swagaswaga iliyopo katika Mikoa ya Dodoma na Singida.
“Tumetenga
maeneo ya uwekezaji katika hifadhi, hivyo tunawaalika sekta binafsi kwa ajili
ya kusaidiana na sisi”, alisema Dkt. Abbasi.
Kadhalika,
Dkt. Abbasi aliipongeza TAWA kwa ujenzi wa miundombinu ya awali katika Hifadhi
ya Swagaswaga ikiwemo ujenzi wa hosteli kwa ajili ya watalii, ujenzi wa Ofisi,
ujenzi wa nyumba za watumishi pamoja na ujenzi wa barabara na alisisitiza kuwa
Wizara itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya utalii
katika maeneo ya hifadhi.
Awali
,akimkaribisha Dkt. Abbasi, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mlage Yussuf Kabange alisema TAWA inaendelea na
mikakati mbalimbali ya utangazaji na uboreshaji wa miundombinu katika Hifadhi
ya Swagaswaga ili kuhakikisha Hifadhi hiyo inafikika kiurahisi zaidi na inaendelea
kupokea wageni wengi zaidi.
Hifadhi
ya Swagaswaga inapatikana takribani kilometa 140 kutoka Mkoa wa Dodoma na
imesheheni vivutio mbalimbali wakiwemo wanyamapori kama vile Tembo, kudu, twiga
na spishi mbalimbali za ndege.
Hifadhi
hii pia imesheheni michoro ya miambani (Mapango yenye alama za kihistoria)
kutoka katika jamii ya Wasandawe.
Na. Joyce
Ndunguru - Dodoma




0 Maoni