Baada ya Hekaheka za wiki nzima, Naibu Waziri Mkuu na Waziri
wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amewasihi watanzania kufanya toba ya
kweli kupata amani.
Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati alipoungana na Wana
Bukombe pamoja na wakazi wa maeneo jirani kumuabudu Mwenyezi Mungu kupitia
Mkesha wa “Ibada Halisi Bukombe Night of Worship” uliofanyika Septemba 20, 2025
katika Uwanja wa Shule ya Msingi Igulwa, Bukombe.
“Uzima tulionao leo ni Wimbo mpya kinywani mwetu, Afya
tulionayo ni Wimbo mpya kinywani mwetu, Hata Bukombe vile tulivyo ni wimbo mpya
kinywani mwetu”.
Ibada hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Ibada Halisi Team na
kanisa AICT Ushirombo imehudhuriwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili
akiwemo Ambwene Mwasongwe, Rehema Simfukwe, Jonathan Kartagata, Joshua Lugendo
na Agape Gospel Band.
0 Maoni