Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Taifa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amewahimiza wananchi wa Jimbo la Sumve,
wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza kuwapigia
kura wagombea wa CCM kwa kuwa Chama hicho kimefanya jitihada kubwa ya kuwaletea
maendeleo.
Dkt.
Biteko amesema hayo Septemba 21, 2025 Mwanza wakati akimnadi mgombea Ubunge wa
Jimbo la Sumve kwa tiketi ya CCM, Moses Bujaga ikiwa ni kuelekea Uchaguzi Mkuu
wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Amesema
Serikali ya CCM imeendelea na jitihada zake za
kujenga Kituo cha Reli ya Kisasa ya SGR kwa ajili ya kupokea mizigo
itakayosafirishwa kwenda maeneo mbalimbali pamoja na kujenga uwanja wa ndege wa
kimataifa jijini Mwanza ili kufungua uchumi wa mkoa huo kwa ujumla.
Aidha,
imehakikisha wananchi wa vijiji vyote katika Jimbo hilo wanapata umeme ikiwa ni
pamoja na usambazaji umeme katika vitongoji.
Dkt.
Biteko ameendelea kusema Dkt. Samia Suluhu Hassan ni msikivu na mtu wa
vitendo zaidi, ambapo katika Jimbo la
Sumve pamoja na miradi mingine amejenga shule za msingi 75, vituo vya afya
vitano pamoja na barabara za lami ili kusafirisha mazao kwa urahisi kufika
sokoni.
“
Maendeleo haya hayasemwi tu yanaonekana na sisi tunataka kuleta maendeleo na
katika kipindi cha miaka mitano ijayo Dkt. Samia anataka kutekekeza miradi
mingi zaidi ya maendeleo. Nawaomba Sumve pigeni kura nyingi kwa wagombea wa CCM
ili kuheshimisha chama chetu na mkimaliza kupiga kura mtudai maendeleo,”
amesisitiza Dkt. Biteko.
Ameongeza
kuwa zoezi la kupiga kura ni la uwekezaji wa maendeleo na kuwa uchaguzi wa
mwaka huu una uhusiano wa moja kwa moja na maisha na maendeleo ya watu. Hivyo
amewataka wananchi hao kumpigia kura mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Akimnadi
mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve kwa tiketi ya CCM, Moses Bujaga, Dkt. Biteko
amemtaja kuwa ni mtu makini, mtulivu na msomi mwenye umahiri katika katika
kutafuta ufumbuzi wa changamoto za wananchi hivyo ifikapo Oktoba 29, wajitokeze
kumchagua kwa kura nyingi.
Naye,
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve, Moses Bujaga
ameishukuru CCM kwa kumteua
kugombea nafasi hiyo na atakapochaguliwa atafanya kazi kwa kushirikiana na
wananchi ili kitimiza jukumu la kuleta maendeleo.
Naye
mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba,
Cosmas Bulala amesema kuwa Kwimba ni kitovu cha maendeleo katika Mkoa wa Mwanza
na kuwa ili kuendelea kupata maendeleo zaidi Oktoba 29 wananchi wawachague tena
wagombea wa CCM.
0 Maoni