WAZIRI
MKUU,Kassim Majaliwa leo Septemba 22, 2025 amefungua maonesho ya nane ya
teknolojia ya madini kwa mwaka 2025 ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya Dkt.
Samia Suluhu Hassan mkoani Geita.
Maonesho
hayo ya Teknolojia ya Madini ambayo yalianzishwa mwaka 2018 yanalenga
kuimarisha sekta ya madini nchini na kuhakikisha kuwa rasilimali madini inawanufaisha Watanzania wote.
Maonesho
hayo yamekuwa jukwaa mahsusi la Serikali, sekta binafsi, wachimbaji wakubwa na
wadogo, taasisi za kifedha, wajasiriamali na wadau mbalimbali wa maendeleo
kukutana, kujadili na kubadilishana uzoefu.
Kaulimbiu
ya Maonesho ya Teknolojia ya Madini kwa mwaka huu wa 2025 ni: “Ukuaji wa Sekta
ya Madini ni Matokeo ya Matumizi ya Teknolojia Sahihi na Uongozi Bora/Shiriki
Uchaguzi Mkuu Oktoba, 2025.”
0 Maoni