Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
amesema mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika uongozi wa Awamu
ya Nane yamechangiwa na kudumu kwa amani, mshikamano na utulivu nchini.
Akizungumza
na jopo la wahariri na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi
alibainisha kuwa mazingira hayo yameiwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa
ya maendeleo kwa ufanisi.
Mambo muhimu aliyoyasisitiza:
Ukusanyaji
bora wa mapato na matumizi sahihi ya fedha za Serikali.
Uwezo wa
Serikali kukopa na kuendesha miradi mikubwa, kutokana na nidhamu ya kifedha na
utaratibu bora wa kulipa madeni.
Uanzishwaji
wa akaunti maalum ya kulipia madeni (Debt Management Account) ambapo Serikali
huweka dola milioni 15 kila mwezi (sawa na dola milioni 180 kwa mwaka).
Kuwekeza
katika maendeleo ya wataalamu wa ndani na kuimarisha vyuo vya amali ili
kuwajengea vijana stadi za kazi za kuajiriwa na kujiajiri.
Kuhusu Uchaguzi Ujao:
Rais Dkt.
Mwinyi amewanasihi viongozi wa dini, wanasiasa na waandishi wa habari kuendelea
kuhubiri amani na mshikamano kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Mkutano huo
umefanyika baada ya jopo la wahariri na waandishi wa habari kutembelea miradi
mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika sekta mbalimbali
Unguja na Pemba.
0 Maoni