Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha Alphonse Simbu kwa kuwa Bingwa wa
Dunia wa mbio za marathon za Tokyo na kwamba ataendelea kutoa kipaumbele katika
sekta ya michezo ili itoe mchango zaidi katika kukuza uchumi wa nchi na
kuongeza wigo wa upatikanaji ajira kwa vijana.
Pongezi
hizo zimetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumamosi (Septemba 27, 2025)
alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla kuwapongeza
wanamichezo na timu zilizofanya vizuri kwenye medani za kimataifa, hafla hiyo
imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel jijini Dar es Salaam.
Katika
tukio hilo Mheshimiwa Majaliwa alitangaza kuwa, Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia
amempatia Mwanariadha Simbu zawadi ya nyumba jijini Dodoma, sambamba na
kikabidhiwa kitita cha shilingi milioni 20 ikiwa ni ishara ya kutambua ushindi
huo ambao umeliletea Taifa heshima kwenye jukwaa la kimataifa.
"Mheshimiwa
Rais Dkt. Samia ameandaa nyumba iliyopo mkoani Dodoma, ambayo itakabidhiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na zoezi hilo
lisichukue muda mrefu kuanzia leo, tusiwe tunatamka ahadi za viongozi halafu
zinakaa muda ambao mtu anajiuliza."
Mheshimiwa
Majaliwa amesema kuwa Mwanariadha Simbu ameandika ukurasa wa upekee kwa kuwa
mtanzania wa Kwanza kutwaa tuzo ya dhahabu katika marathoni ya Dunia ya mwaka
2025 "Haya ni Mashindano makubwa zaidi ya riadha duniani baada ya Michezo
ya Olympic, yakihusisha wanariadha Bora kutoka Mataifa yote duniani."
Amesema
kuwa Serikali mara zote umekuwa ikiweka jitihada za kutosha za kuhakikisha
sekta ya Michezo inakuwa na mchango kwa Taifa "Matokeo tunayoyashuhudia
hivi sasa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ikiwemo
ukarabati wa viwanja na kuongezwa kwa bajeti kutoka shilingi bilioni 38 mwaka
2022 Hadi bilioni 326 mwaka 2025/2026."
Katika
hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wanamichezo nchini kuweka
jitihada binafsi katika kushiriki katika michezo kwani ushindi unaweza
kupatikana kwa kuweka nia "Wekeni mikakati ya ushindi ili muweze
kuipeperusha bendera ya Taifa letu kimataifa".
Naye RAIS
wa Shirikisho la Riadha Tanzania (SRT) Rogath Stephen ameishukuru Serikali kwa
namna inavyotoa mchango kubwa kwa vyama na namna anavyoendeleza Michezo.
"Hatujawahi kufanyiwa mambo ambayo kwasasa yanafanyika, kupitia Serikali
tumekuwa tunahudumiwa kwa namna ya kipekee."
Kwa
Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson
Msigwa amesema kuwa Medali ya dhahabu ya Alphose Simbu imefanikiwa kupata tiba
ya kiu ya Watanzania ya kupata Medali za dhabau katika michezo ya kimataifa.
"Hii imewezekana kutokana na na maamuzi ya viongozi wetu kuwa na maono ya
kurudisha heshima kwa Taifa baada ya kufanya uwekezaji mkubwa mchezoni."
Ameongeza
kuwa Kiu kubwa iliyobaki ni kuhakikisha watanzania wanapata medali kwenye
Michezo ya Olympic pamoja na michezo ya jumuiya ya madola "Sisi kama
Serikali tumejipanga kuhakikisha tunafanikiwa kuleta medali hizi hapa nyumbani,
tunaweka mikakati imara ya usimamizi, kwa sasa kuwa wasindikizaji imetosha,
Tunaamini mwakani tunaweza kupata media kwenye Michezo ya jumuiya ya madola na
2028 tutapata medali kwenye Olympic."
Timu
nyingine zilizopongezwa na kupewa zawadi ya shilingi milioni kumi ni Timu ya
Taifa ya Futsal ya Wanawake ambayo imefuzu kushiriki kombe la dunia
(Philippines 2025), Timu ya JKT Queens ambao ni mabingwa wa Mashindano ya CAF
Woman's Championship League Cecafa Qualifiers 2025.
Timu
nyingine ni timu ya Taifa ya Cricket U-19
ambayo itashiriki mashindano ya Dunia 2026 nchini Zimbabwe na timu ya
wenye ulemavu (Tembo Worriers) ambao wamekuwa mshindi wa Pili wa Michezo
ya Afrika Mashariki na Kati.

0 Maoni