Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele jana
Septemba 22, 2025 ametembelea Halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika Jimbo la
Iringa Mjini na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo
jimbo la Kilolo Mkoani Iringa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya
kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Pamoja na
mambo mengine Jaji Mwambegele alipokea taarifa ya majimbo hayo kutoka kwa
wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari
vimepokelewa katika Halmashauri hiyo.
Jaji
Mwambegele pia alipata fursa ya kushuhudia Kampeni za Mgombea wa Kiti cha Rais
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama
cha Makini (MAKINI), Mhe. Coster Jimmy Kibonde na Mgombea Mwenza, Mhe. Aziza Haji Suleiman waliokuwa katika Mkutano
wa Kampeni Stendi ya Zamani ya Mkoa wa Iringa majira ya Saa 10 jioni.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa
kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
"Kura
Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"
0 Maoni