MAANDALIZI ya mikutano ya kampeni ya Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
Samia Suluhu Hassan, mkoani Ruvuma yamekamilika.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma,
Oddo Mwisho, amethibitisha hilo leo Septemba 20, baada ya kukagua maandalizi
hayo akiwa ameambatana na Mgombea Mwenza, Dkt. Emmanuel John Nchimbi.
Amesema maandalizi yote muhimu
yamekamilika kwa ajili ya kumpokea mgombea huyo.
Kwa mujibu wa Oddo, Dkt. Samia
anatarajiwa kuwasili kesho Septemba 21 katika Uwanja wa Ndege wa Songea, ambapo
atapokelewa na Mgombea Mwenza Dkt. Emmanuel John Nchimbi, viongozi wa chama
pamoja na wananchi wa mkoa huo.
Ziara yake itaanzia wilayani
Nyasa, ikiwemo kusimama Mbinga kuzungumza na wananchi na kisha kufanyika
mkutano mkubwa wa kampeni katika eneo la Mbamba Bay.
Aidha, Septemba 22 Dkt. Samia
atahutubia mkutano mkubwa wa kampeni mjini Songea katika Viwanja vya VETA
vilivyopo Msamala, kabla ya kuelekea Namtumbo na Tunduru ambapo atafunga ziara
yake ya kampeni mkoani humo.
Baada ya hapo, Septemba 23
ataanza kampeni mkoani Mtwara.
0 Maoni