MGOMBEA
Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Joh Nchimbi leo Septemba 28,2025 amefanya
mkutano mkubwa wa kampeni katika Uwanja
wa Mwenbe Yanga jijini Dar es Salaam.
Katika
mkutano huo,Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kuwanadi baadhi ya wagombea
Ubunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa jimbo la Temeke,Ndugu Mariam Kisangi
pamoja na Madiwani.
Dkt.Nchimbi
ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 29, 2025 wakipeperusha bendera ya CCM.
Mpaka
sasa mkoa wa Dar es Salaam unakuwa wa
15 kufikiwa na Dkt Nchimbi katika kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Mgombea Urais wa chama hicho
Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge pamoja na Madiwani.



0 Maoni