Kapteni Abbas Mwinyi afariki dunia

 

Mtoto wa aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi, Kapteni Abbas Mwinyi amefariki dunia leo Septemba 25  katika Hospitali ya Lumumba Mjini Unguja, Zanzibar.

Kapteni Abbas Ali Mwinyi ni kaka wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Abbas Ali Mwinyi alikuwa mbunge aliyemaliza muda wake na mgombea wa jimbo la Fuoni. Taarifa rasmi na taratibu za maziko zitatolewa baadae na familia. 

Chapisha Maoni

0 Maoni