Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt Hussein Ali Hassan
Mwinyi ametangaza kwa masikitiko kutokea kifo cha Kaka yake Kapteni Abbas Ali
Hassan Mwinyi aliyefariki dunia leo 25 Septemba 2025 Mjini Unguja, Zanzibar.
Ibada ya
kumsalia Marehemu itafanyika katika Msikiti wa Zanzibar - Msikiti wa Qaboos
baada ya sala ya Ijumaa na baada ya hapo maziko yanafanyika Mangapwani katika
eneo ambalo amezikwa Mzee Ali Hassan Mwinyi, ambapo watu waliopo maeneo ya
Mangapwani, Bumbwini, Fujoni na maeneo ya karibu watapata kutabaruku kabla ya
kuzika.
Visomo
Msikitini vitaanza saa 4 asubuhi.
Kapteni Abbas
Ali Mwinyi alikuwa mbunge aliyemaliza muda wake na mgombea wa jimbo la Fuoni
kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

0 Maoni