Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amefanya kampeni za nyumba kwa
nyumba ili kutafuta kura za kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na
wabunge na madiwani, ili waweze kuwaletea wananchi maendeleo.
Kampeni
hizo zimefanyika katika Kijiji cha Kakobe, Kata ya Kazunzu, kabla ya uzinduzi
rasmi wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Nyambeba, Jimbo la Buchosa.
Shigongo
amewaomba wananchi wa Buchosa kushirikiana kwa pamoja katika kutafuta kura za
rais, wabunge na madiwani wanaotokana na CCM, kwa lengo la kuhakikisha chama
hicho kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu.
Amesema
wagombea wa CCM ndiyo chaguo bora kwa Watanzania kutokana na kazi nzuri
zilizofanywa na serikali ya CCM na zinazondelea kufanyika, hivyo kuna sababu ya
kuendelea kukiunga mkono chama hicho ili kiendelee kuiongoza Tanzania.
0 Maoni