Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa
ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele Septemba 19, 2025
ametembelea Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika Majimbo ya Uchaguzi ya Mbeya
Mjini na Uyole na kupokea taarifa ya mkoa kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa
Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari
vimepokelewa katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Jaji Mwambegele pia alipata fursa
ya kutembelea kampeni za wagombea Ubunge wa chama cha CUF na CCM katika majimbo
hayo.
Kwa mujibu wa ratiba
iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba
29, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa
ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa
Uchaguzi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya ambapo alisisitiza uadilifu wakati
wa utendaji kazi wao.
0 Maoni