Mgombea mwenza wa Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi
amewasili Songea, mkoani Ruvuma leo Septemba 19, 2025.
Dk Nchimbi ataungana tena na
Mgombea urais wa chama hicho, Dkt.Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwasili
kesho ambapo watakutana mkoa mmoja tangu Agosti 28, mwaka huu walipozindua
kampeni za chama hicho kitaifa mkoani Dar es Salaam.
Baada ya uzinduzi,Dkt. Samia na
Dk Nchimbi waligawana maeneo kwenda kunadi Ilani ya CCM na kueleza kile
walichokifanya miaka mitano iliyopita na wanachotarajia kukifanya endapo
watachaguliwa.
Baada ya uzinduzi, Samia yeye
alianzia Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora,
Kigoma na mikoa mitatu kati ya mitano ya Zanzibar ambayo ni, Kusini Unguja,
Kaskazini Unguja na Kusini Pemba.
Dk Nchimbi yeye alianza kwa
watani zake kanda ya ziwa mikoa wa Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita,
Kagera, Rukwa, Katavi, Arusha, Kilimanjaro, Tanga na sasa anaingia
nyumbani mkoani Ruvuma.
0 Maoni