Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewahutubia
wananchi wa jimbo la Lupembe, waliohudhuria
mkutano wake mdogo wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa mpira wa
Ilunda, Lupembe leo Jumatano Septemba 24, 2025 mkoani Njombe.
Pamoja na mambo mengine Dkt. Nchimbi alitumia
mkutano huo kuwanadi mgombea ubunge wa jimbo la Lupembe kwa tiketi ya CCM, Ndugu
Edwin Enosy Swallel Swallel pamoja na madiwani wa jimbo hilo.
Dkt. Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni
nchi nzima, kusaka kura za ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwaombea
kura Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na
Madiwani.



0 Maoni