MGOMBEA
mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewahutubia Wananchi wa Mjini Njombe,waliohudhuria mkutano wake wa
hadhara wa kampeni huku akiwaomba ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wakipigie kura
Chama hicho ili kishinde kwa kishindo.
Dkt. Nchimbi
ameyasema hayo leo Septemba 23,2025 alipokuwa katika uwanja wa Stendi ya
zamani, mkoani Njombe ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa ahadi kwa wananchi wa
Njombe endapo wataichaguwa CCM basi
Ilani ya chama chake imepanga kufanya mipango mingi ya maendeleo mkoani humo.
Maendeleo
hayo ni katika maeneo mbalimbali yakiwemo katika sekta ya afya, elimu, kilimo,
maji pamoja na kuinua biashara
mbalimbali.
Pia Dkt. Nchimbi
alitumia nafasi hiyo ya kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Jombe Mjini,Ndugu
Deodatus Philip Mwanyika pamoja na Madiwani wa jimbo hilo.
Dkt.
Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni nchi nzima, kusaka kura za
ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),ambapo mpaka sasa
amefika mikoa 13.



0 Maoni