MGOMBEA
Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
amewahutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ambapo ametumia nafasi
hiyo kuwaomba kumpigia kura za kishindo mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia
Suluhu Hassan, wabunge na madiwani.
Dk.Nchimbi ametoa ombi hilo leo Septemba 3,2025
alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara
ambapo katika mkutano huo amewanadi Wabunge
wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas
Katambi.
Wengine
ni Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu, Lucy
Mayenga , Jimbo la Solwa Ahmed na Itwangi na Azza Hillal pamoja na madiwani.
Dkt. Nchimbi
ameendelea kunadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi
imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika
miaka mitano ijayo.
Aidha
amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba
wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na
Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
0 Maoni