MGOMBEA Mwenza wa Urais wa kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameendelea kunadi Ilani ya Chama hicho ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo
kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo
katika miaka mitano ijayo.
Dk. Nchimbi leo Septemba 9,2025 amewasili mkoani Katavi na kuhutubia wananchi katika Uwanja wa Maridadi,Mpanda mjini,
kwenye mkutano wake wa hadhara wa Kampeni akitokea mkoani Rukwa.
Baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mpanda Mjini,Balozi Nchimbi
amewanadi Wagombea Ubunge wa majimbo
mbalimbali ya Mkoa huo,akiwemo Mbunge wa
jimbo la Mpanda mjini, Haidary Hemed Sumry pamoja na Madiwani.
Awali, Dk. Nchimbi amewahutubia wananchi wa Majimoto,katika
jimbo la Kavuu mkoani Katavi na kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Laurent
Deogratius Luswetula pamoja na Madiwani.
Akiwa katika mkutano huo Dk. Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Dk.Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
0 Maoni