Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema kuwa wananchi
wanahitaji huduma na maendeleo
yanayotokana na utekelezaji wa mipango thabiti na sio kwa maneno
yasiyotekelezeka.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Septemba 11, 2025 wakati wa
mkutano wa kampeni katika Kata ya Butinzya wilayani Bukombe mkoani Geita.
“ Hawa wananchi wanataka huduma hawataki maneno kazi yangu
ni kusogeza huduma kwa watu, nataka
mgombea udiwani Mathias hii Zahanati ya Butinzya ikamilike katika
kipindi cha miezi mitatu baada ya kuchaguliwa,” amesema Dkt. Biteko
Amesisitiza “Tunahitaji ukamilishaji wa haraka nimenunua vifaa,
nataka tumalize hapa tuangalie kitu kingine. Tuna mpango wa kujenga vituo vya
afya 59 katika Wilaya Bukombe.”
Ameendelea kusema wamejenga barabara ya lami na wanataka
wananchi wa Kata hiyo wapite kwenye barabara hiyo za lami kwenda Ushirombo na
maeneo mengine, umeme ufike kwenye vitongoji vyote huku akisisitiza kuwa
mipango ya maendeleo hailetwi kwa kusema sana na kuwa CCM wanatekeleza mipango
hiyo kwa vitendo.
Fauka ya hayo, amesema Rais Samia ametoa fursa kwa wananchi
kufanya maendeleo Bukombe akitolea mfano kuruhusu wananchi kuchimba madini
katika Pori la Kigosi.
“ Mambo yanaenda kwa sababu Rais Samia anatupenda na sasa
utaona maendeleo Bukombe kwa sababu ametoa fursa ili watu wapate maendeleo,
niwaombe Oktoba 29 mwaka huu tumpigie kura nyingi, watu wote tujitokeze kupiga
kura,” ameongeza Dkt. Biteko.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe, Matondo
Kihanja Lutonja amewaomba wananchi wa Kata hiyo kuwapigia kura wagombea wa CCM
kwa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani kwa kuwa CCM ina dira inayotekelezeka na
hivyo wakiamini chama hicho ili kiendelee kushika dola na kutumiza matarajio
yao na ya Watanzania kwa ujumla.
Mgombea wa Udiwani Kata ya Butinzya, Kwizi Mathias
amemshukuru Dkt. Biteko kwa kuhakikisha kuwa katika uongozi wake
miradi ya maendeleo imetekelezwa katika Kata hiyo ikiwemo ya afya na
barabara.
Aidha, ameahidi kuwa akichaguliwa atawaletea maendeleo
wananchi wa Kata hiyo.



0 Maoni