Wenyeviti wa Bodi za
Taasisi za Uhifadhi zinazounda Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu Tanzania wakiongozwa
na Mwenyekiti wao Jenerali (Mstaafu) George M. Waitara (Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini TANAPA) wamekutana leo Agosti 4, 2025 Jijini, Dar es Salaam katika
kikao cha kawaida cha kujadili mwenendo wa Jeshi la Uhifadhi na Misitu Nchini.
Kikao hicho pia,
kimehudhuriwa na Jenerali (Mstaafu) Venance S. Mabeyo (Mwenyekiti wa Bodi ya
Ngorongoro), Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R.Semfuko (Mwenyekiti wa Bodi ya
TAWA) pamoja na Meja Jenerali Mbaraka N. Mkeremi (Mwenyekiti wa Bodi ya TFS).
Aidha, pamoja na
Wenyeviti hao, kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kamishna wa Uhifadhi - TFS
Prof. Dosantos Silayo, Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA, Musa Nassoro Kuji, Kamishna
wa Uhifadhi - Ngorongoro, Abdul- Razaq Badru, Kaimu Kamishna wa Uhifadhi -
TAWA, Mlange Kabange pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi,
Fidelis Ignas Kapatala ambaye ni Mratibu wa Jeshi la Uhifadhi na Misitu katika
Wizara ya Maliasili na Utalii.
0 Maoni