Wajumbe wa Mkutano Mkuu
na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe wamemchagua mtia
nia wa jimbo hilo Dkt. Doto Mashaka Biteko kwa asilimia 99.8 baada ya kupata
kura 7,441 kati ya kura 7,456 zilizopigwa ili apeperushe bendera ya Chama
hicho.
Akitangaza matokeo hayo Agosti
04, 2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Jimbo la Bukombe linajumla ya wajumbe
7,835 na waliopiga kura ni 7,456 ambapo kura zilizoharibika ni 15, kura za
hapana ni 0, kura halali zilizopigwa ni 7,441.
Kwa matokeo hayo, Dkt.
Doto Mashaka Biteko amepata kura 7,441 kati ya 7,456 sawa na wastani wa
asilimia 99.8 uchaguzi uliofanyika katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.
0 Maoni