Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaanza kuwatoza kodi wafanyabiashara za mtandao wakiwamo wanaopangisha nyuma zao kwa malazi maarufu kama Air BnB ambapo wamepewa muda hadi Septemba Mosi kuanza kujisajili.
Hayo yameelezwa na Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Juma
Mwenda katika Semina ya Kutoa Elimu ya Kodi na Kuwawezesha Wafanyabishara wa
Mtandaoni iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa
wafanyabiashara, mabenki pamoja na wahariri wa vyombo vya habari nchini.
“Kwa wafanyabiashara wa mitandaoni wakiwamo wanaopangisha
nyuma zao kwa malazi maarufu kama Air BnB lazima wajisajili ili waanze kulipa
kodi, ila kwa wafanyabiashara wadogo wa mitandao wao tutawapa muda kidogo wa
kuwaelimisha kwanza kabla ya kuanza kulipa kodi,” alisema Bw. Mwenda.
Kamishna Mwenda ameeleza kuwa kwa
mfanyabiashara wa mtandaoni ambaye anafanyanya biashara yake, ambapo mapato
yake kwa mwaka hayapungui shilingi 4,000,000, anapaswa kulipa kodi ya shilingi
100,000 tu kwa mwaka.
“Lakini hata yule ambaye mapato yake yanafikia
shilingi 11,000,000 kwa mwaka atachangia kodi ya shilingi 250,000 tu kwa mwaka,
ukiigawa kwa nyie mnao jua mahesabu ni mchango mdogo tu na mtu anajisikia sifa
kuwa na yeye anachangia miradi ya maendeleo,” alisema Bw. Mwenda.
Awali Kamishana wa Kodi za Ndani Bw. Alfred Mregi
alisema kutokana na kukua kwa teknolojia mazingira ya kufanyabiashara nayo
yamebadilika na sasa wapo wafanyabiashara ambao nao wanafanyabiashara kwa njia
ya kidigitali (mtanaoni) kama vile instagram, airbnb, Booking.com na kadhalika.
“Majukwaa hayo ya mtandaoni ni fursa kwa Watanzania
kuongeza kipato kwa ajili ya ustawi wa biashara zao na taifa kwa ujumla,” alisema
Bw. Mregi.
Amesema
kutokana ukuaji wa biashara za mtanaoni ambao ni mfumo mpya wa biashara
uliosababishwa na ukuaji wa teknolojia, TRA imeona vyema kutoa elimu katika
eneo hilo ili wafanyabiashara wa kundi hilo waongeze uelewa utakaosaidia kutimiza
wajibu wao wa kikodi kwa usahihi na kuzingatia mapato ya kisheria.
0 Maoni