Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya
Viongozi Wanawake (WPL), Bi. Neema Lugangira amevitaka vyombo vya habari nchini
vitumie Akili Unde kwa uadilifu na isiwe
silaha ya kupotosha demokrasia katika kipindi cha uchaguzi mkuu nchini.
Bi. Lugangira ambaye anaitumikia
Jumuiya hiyo inayohusisha Marais, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Mawaziri,
Wabunge na Mameya, yenye maskani yake Brussels nchini Ubelgiji, ametoa kauli
hiyo leo kwenye Mkutano wa Wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Amesema kwamba Akili Unde imeleta
changamoto za Deepfakes (picha na video bandia) zinazoweza kuharibu heshima ya
mgombea, Bots (roboti) zinazopandikiza
maoni bandia pamoja na mashambulizi ya matusi na ukatili wa kijinsia mtandaoni.
Hata hivyo, amesema Akili Unde pia ni fusa inaweza kutumika vizuri
kama kutumika kufuatilia mwenendo wa hate speech (kauli za chuki) mtandaoni,
kusaidia kuzuia upotoshaji wa uchaguzi.
“Akili Unde pia Inaboresha
ushirikishwaji wa wapiga kura na elimu, kwa kutoa taarifa kwa urahisi kuhusu
mchakato wa uchaguzi, sheria, na wagombea kwa kutumia roboti za mazungumzo
(chatbots),” alisema Lugangira.
Ameongeza kuwa Akili Unde inasaidia
kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wapiga kura wa makundi maalum, kama vile
walemavu na vijana, kwa kutumia teknolojia ya sauti na huduma za kielektroniki.
Pamoja na mambo mengine, amesema Akili
Unde pia inaweza kuboresha mikakati ya kampeni kwa kutumia uchambuzi wa data ya
wapiga kura na kufanya matangazo ya kisiasa kuwa ya kulenga na yenye ufanisi.
Bi. Lugangira amesema vyombo vya
habari vina jukumu kubwa la kulinda uchaguzi dhidi ya matumizi mabaya ya teknolojia
kwa pamoja na kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa fursa sawa, ukosefu wa usawa
na ukatili wa kijinsia unaoripotiwa na kushughulikiwa.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya
Viongozi Wanawake (WPL), Bi. Neema Lugangira akiwakabidhi nakala za Mwongozo wa Uchaguzi Afrika wa
Mitandao ya Jamii kwa Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile na Makamu Mwenyekiti
Dkt. Bakari Machumu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya
Viongozi Wanawake (WPL), Bi. Neema Lugangira akiwakabidhi nakala za Mwongozo wa Uchaguzi Afrika wa
Digitali na Mitandao ya Jamii kwa Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile na Makamu
Mwenyekiti Dkt. Bakari Machumu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya
Viongozi Wanawake (WPL), Bi. Neema Lugangira akiwakabidhi nakala za Mwongozo wa Uchaguzi Afrika wa
Digitali na Mitandao ya Jamii kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari
Wanawake Tanzania (TAMWA) Dkt. Rose Rueben na aliyekuwa Mwenyekiti wa TAMWA Bi.
Joyce Shebe.
0 Maoni